Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi umeratibu ziara ya timu ya Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Banjamin Mkapa iliyoongozwa na Mkurugezi Mtendaji Hospitali hiyo Prof. Abel Makubi. Timu hiyo imetembelea Hospitali zilizopo Mkoa wa kusini, Kati na Kaskazini mwa Malawi kwa lengo la kujionea huduma za kibingwa zinazohitajika ili kuandaa na kufanikisha kambi ya matibabu. Vilevile, kuanzisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja kufanya tafiti za pamoja. Tarehe 19 Desemba 2025 timu hii ilikutana na kufanya mazungumzo na katibu Mkuu Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Malawi Dr. Dan Namarika, pamoja na kukubaliana kufanyika kwa kambi ya Matibabu nchini Malawi kabla ya mwisho wa mwezi Machi 2026; imekubalika pia kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya pamoja na baadhi ya Madaktari kutoka Jamhuri ya Malawi watakwenda kutembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa lengo la kujionea jinsi Hospitali hiyo na Hospitali nyingine nchini zilivyopiga hatua katika matibabu ya kibingwa. Aidha,kujionea jinsi Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyowekeza katika miundo ya kisasa ya Huduma za Afya. Hatua hii ni katika kutangaza Utalii wa Tiba utakaowezesha kusainiwa kwa makubaliano ya kuwawezesha wagonjwa kutoka Malawi kuja kutibiwa mchiniTanzania.


