Mnamo tarehe 10 Juni 2026, Mhe. Agnes Richard Kayola, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Malawi, alifanya mazungumzo ya kimkakati na Dkt. Albert Komba, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la kimataifa lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Program for Appropriate Technology in Health (PATH). Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha diplomasia ya afya na uchumi kwa kutumia
Katika kikao hicho, Dkt. Komba alifafanua kuwa ujio wake nchini Malawi ni kutokana na nchi hiyo kuwa kati ya nchi zinazonufaika na miradi ya PATH na uhitaji mkubwa wa usaidizi wa kitaalam ili kuweka mifumo ya sekta ya afya ya jamii kuweza kuhimili changamoto za kiuchumi na miundombinu.
Alifafanua zaidi kuwa, jukumu kuu la PATH ni kuratibu na kushawishi taasisi kubwa za ufadhili wa kimataifa kama _American Heart Association, Unitaid fund , na Prevail Fund kuelekeza uwekezaji na miradi ya maendeleo katika nchi zenye uhitaji ikiwemo Malaw
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Kayola alibainisha kuwa nchi ya Malawi inao uhitaji mkubwa wa wataalamu wa tiba na mifumo ya uhakika ya usambazaji dawa.
Katika hatua nyingine, Mhe.Balozi Kayola, aliongeza kuwa, katika kutekeleza diplomasia ya uchumi na utalii wa
kimatibabu, Ubalozi tayari umeratibu na utaendelea kuratibu kambi za matibabu ya kibingwa
nchini Malawi kwa kushirikiana na Hospitali ya Benjamin Mkapa ya
Tanzania, kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kimkakati na ujirani mwema kati ya Tanzania na Malawi.

