Leo, terehe 23 Mei,2024, Ubalozi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania nchini Malawi umeshiriki kwenye ufunguzi wa Maonesho ya 34 ya Kimataifa ya Biashara ya Malawi yaliyofanyika jijini Blantyre.

Mgeni rasmi kwenye Maonesho haya alikuwa Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera, Rais wa Jamhuri ya Malawi.

Wakati wa maonesho hayo, Mheshimiwa Rais Chakwera alitembelea baadhi ya mabanda ya maonesho ikiwemo Banda ya Ubalozi pamoja na Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania  (TPA). Ubalozi pamoja na Ofisi ya TPA walimpatia Mhe. Rais Chakwera zawadi ikiwemo Tshirt na kofia za TPA, Majani ya Chai, Kahawa na Korosho.

Sambamba na hilo, waandaji wa maonesho haya, waliandaa vigezo vya kumpata mshiriki bora wa maonesho ya 34 ambapo Ofisi ya Uwakilishi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeshinda Tuzo ya Mshiriki Bora wa kimataifa (International Exhibitors Award) wakati wa maonesho hayo.