Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameanza ziara ya kiserikali nchini Malawi tarehe 5 Julai 2023. Akiwa ziarani hapa nchini Malawi alipokelewa na Mwenyeji wake Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera, Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mke wa Rais, Mhe. Monica Chakwera pamoja na viongozi wengine wa Serikali katika Uwanja wa Kimatafa wa Kamuzu, Mkoa wa Kati Lilongwe.
Baada ya mapokezi rasmi alipata alitembelea Ofisi za Jiji la Lilongwe ambapo pamoja na mambo mengine alikabidhiwa Mfano wa Funguo kuashiria kumpatia uhuru wa kutembelea Jiji la Lilongwe wakati wowote. Baadae jioni alialikwa kushiriki kwenye Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa maalum kwa ajili yake.
Leo tarehe 6 Julai 2023, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alitembelea Bunge la Jamhuri ya Malawi ambapo alipokelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Saulos Klaus Chilima, Spika wa Bunge la Malawi, Mhe. Catherine Gotani Hara, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Malawi pamoja na viongozi wengine wa Serikali. Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na mambo mengine, alipanda mti katika eneo la Bunge. Vilevile, alitembelea Kaburi ya Hayati Kamuzu Hasting Banda, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Malawi ambapo aliweke shada la maua. Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan baadae leo atakuwa Mgeni Rasmi kwenye Sherehe Rasmi za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Jamhuri ya Malawi.